Jumapili 21 Juni 2026 - 16:15
Vita vya Hivi Karibuni vya Marekani na Israel dhidi ya Iran si Vita vya Nchi Moja, Bali ni Mapambano ya Umma Mzima wa Kiislamu

Hawza/ Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad, huku akisisitiza kuhusu sura pana ya makabiliano ya hivi karibuni kati ya Marekani na Israel dhidi ya Iran, ameeleza kuwa; mzozo huu si vita vya nchi moja pekee, bali ni mapambano kamili ya Umma wa Kiislamu kwa ajili ya kulinda uhuru wake, heshima yake na mustakabali wake.

Kwa mujibu wa Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Yasin Mousawi, Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad na mmoja wa walimu mashuhuri wa Hawza ya Najaf Ashraf, huku akizungumzia maendeleo ya hivi karibuni ya kisiasa na kijeshi, amesema: Maendeleo haya yanaonesha mabadiliko muhimu katika mwenendo wa mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani, na Tehran imesitisha ushiriki wake katika duru mpya ya mazungumzo kwa kupinga kuendelea kwa operesheni za kijeshi za utawala wa Kizayuni nchini Lebanon.

Katika khutba ya Swala ya Ijumaa, huku akieleza kuwa habari muhimu zaidi katika medani ya kisiasa na vyombo vya habari ni kukubaliwa kwa masharti kumi na manne (14) na Donald Trump, Rais wa Marekani, alisema: Trump amekubali masharti hayo yaliyowasilishwa na ujumbe wa mazungumzo wa Iran na ametia saini hati inayojulikana kama “Mkataba wa Maelewano” kwa lengo la kufikia makubaliano ya mwisho ndani ya muda maalumu.

Ayatullah Mousawi aliongeza: Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kutoridhishwa kwa baadhi ya makundi ya Republican na Democratic, kiasi kwamba makubaliano haya yameelezwa na wao kuwa ni “kushindwa kwa Marekani katika mazungumzo na Iran kutoka ikiwa na mkono wa juu.”

Akizungumzia msimamo wa utawala wa Kizayuni, alifafanua: Msimamo wa utawala huo unapinga kikamilifu makubaliano haya, na viongozi wake wanayaona kama kushindwa kwa kisiasa na kijeshi; ndiyo maana wanasisitiza kuendeleza vita na kuvuruga au kusitisha aina yoyote ya maelewano.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad pia alibainisha kuwa; Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni, kwa vitendo hajazingatia vipengele vya makubaliano hayo, na licha ya mashinikizo ya Marekani ameendelea kuongeza mvutano wa kijeshi. Miongoni mwa hayo ni matukio ya kusini mwa Lebanon na eneo la “Ali al-Tahir” kaskazini mwa Nabatiyah, ambapo juhudi za majeshi ya Israel kusonga mbele zilikabiliwa na majibu makali kutoka kwa Muqawama wa Lebanon, jambo lililosababisha kuuawa na kujeruhiwa idadi ya maafisa na wanajeshi wa utawala huo.

Alisisitiza kuwa; msimamo wa Iran tangu mwanzo umekuwa wazi, na kwamba sharti lake kuu ni kusimamishwa kikamilifu kwa mapigano katika medani zote za Mhimili wa Muqawama kabla ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote ya mwisho. Kwa mujibu wake, Tehran imewaeleza wapatanishi kuwa haitashiriki katika mazungumzo ikiwa mashambulizi dhidi ya Lebanon katika nyanja za ardhini, baharini na angani hayatakoma.

Ayatullah Mousawi aliongeza kuwa; Iran ilikuwa tayari kushiriki katika duru mpya ya mazungumzo, lakini kutokana na maendeleo ya hivi karibuni kusini mwa Lebanon, ilisimamisha mchakato huo. Kwa sasa hali ipo kati ya njia mbili: ima kuongezeka kwa mapigano, au Marekani kuweka shinikizo la kweli kwa utawala wa Kizayuni ili utekeleze usitishaji vita na kujiondoa.

Akisisitiza asili ya vita hivi alisema: Makabiliano haya “si vita vya Iran peke yake,” bali ni “vita vya Umma wa Kiislamu, historia yake na mustakabali wake.” Aliongeza kuwa; vita hivi ni mapambano ya kulinda dini safi, uhuru, kujitegemea na heshima, na haviishii katika nchi moja maalumu.

Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Baghdad alifafanua kuwa; Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haijatetea tu watu wake, bali pia imeunga mkono Ghaza, Lebanon, Syria na Iraq, na imesimama pamoja na mataifa yanayokabiliana na ugaidi na uvamizi kwa mujibu wa wajibu wake wa kidini na kimaadili.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha